Asili Yetu

Kuhusu JKQZ

Fahamu historia, maono, dhamira, na viongozi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Zanzibar.

Historia Yetu

Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Zanzibar (JKQZ) iliasisiwa kwa lengo madhubuti la kusimamia, kuendeleza, na kuhamasisha hifdhi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika visiwa vya Zanzibar na maeneo jirani.

Kwa zaidi ya miongo kadhaa, tumekuwa kiungo muhimu katika kuunganisha vituo vya kuhifadhisha Qur'an (Madrasa), waalimu, na wanafunzi ili kujenga mfumo mmoja imara unaotambulika kimataifa.

"Tumeandaa mashindano mengi makubwa kuanzia ngazi ya shule, wilaya, mkoa, hadi taifa, na kuzalisha mahafidh wanao ipeperusha bendera yetu."
20+Miaka ya Huduma

Maono Yetu

Kuwa kituo kikuu na cha mfano barani Afrika katika kulea, kusimamia, na kuzalisha wasomi na mahafidh wa Qur'an Tukufu wenye uelewa mpana na maadili mema.

Dhamira Yetu

Kuhakikisha vizazi vya sasa na vijavyo vinapata fursa sawa na mazingira bora ya kusoma, kuhifadhi, na kufanyia kazi mafundisho ya Qur'an kupitia mashindano na matukio jumuishi.

Makusudio

Malengo Yetu Makuu

Kukuza Usomaji

Kuhamasisha usomaji sahihi wa Qur'an kwa kufuata kanuni za Tajweed.

Kujenga Maadili

Kutumia mafundisho ya Qur'an kujenga kizazi chenye hofu ya Mungu na maadili mema.

Kuunganisha Jamii

Kuweka umoja miongoni mwa waislamu kupitia mikusanyiko ya mashindano na usomaji.

Uongozi

Bodi na Viongozi Wetu

Watu waliojitolea kuhakikisha harakati za JKQZ zinafika mbele na kuwanufaisha wengi.